Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Didier Gomes Da Rosa amesema kuwa hawezi kujiunga na Young Africans.

Kocha Gomes ametoa kauli hiyo alipoongea na wanahabari jana Jumanne (Oktoba 26) majira ya jioni, baada ya kujiuzulu nafasi yake Simba SC.

Kocha huyo kutoka nchini Ufaransa amesema suala la kufanya kazi kwenhe timu pinzani haliwezekani kama ilivyo katika nchi zingine duniani, ambapo kocha fulani hawezi kufundisha timu ya upande wa pili.

“Kocha wa PSG hawezi kuwa kocha wa Marseille, hata Hispania Kocha wa Barcelona hawezi kuwa kocha wa Madrid.” amesema Gomes

Katika hatua nyingine Kocha Gomes amethibitisha taarifa za kuwa na ofa za klabu kadhaa, hivyo anaendelea kufanya mazungumzo na wakala wake.

“Nimepokea ofa miezi mitatu iliyopita, nitaangalia na wakala wangu, siwezi kuongea sana kuhusu hayo.” amesisitiza Gomes

Kocha Gomes anaondoka Simba SC baada ya kikosi chake kukubali kufungwa dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana mabao 3-1, na kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2021/22.

Magori: Wapuuzeni wenye nia ovu
Donny asaka njia ya kuondoka Old Trafford