Inaelezwa kuwa Kocha wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Didier Gomez hakuwepo kwenye mazoezi ya kikosi chake jana jioni katika uwanja wa Boko Veterani.

Kikosi cha Simba SC kinajiandaa na mchezo wa Ligi Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22, dhidi ya Polisi Tanzania, utakaochezwa kesho (Jumatano) Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja jioni.

Taarifa zinaeleza kuwa Kocha huyo kutoka nchini Ufaransa, hakuonekana kabisa mazoezi, sambamba na Kocha wa Makipa, Milton Nienov na Kocha wa mazoezi ya viungo Adel Zrane.

Kutokuonekana kwa makocha hao, kunaendelea kutoa kiashirikio kibaya ndani ya Simba SC, ambapo tetesi zinasema huenda Uongozi ukamtimua kazi Kocha Gomes na wasaidizi wake, kufuatia matokeo ya kupoteza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana Jumapili (Oktoba 24).

Simba SC ilipoteza mchezo huo, kwa kufungwa mabao 3-1 na kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa faida ya mabao mengi waliyoipata Jwaneng Galaxy.

Mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Jumapili (Oktoba 17) mjini Gaborone, Simba SC ilichomoza na ushindi wa mabao 2-0.

Jaji mpya kesi ya kina Mbowe
HESLB waweka hadharani wanufaika mkopo chuo kikuu