Saa chache kabla ya mpambano wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya Makundi kati ya AS Vita Club dhidi ya Simba SC, kocha Didier Gomes amesema anamtambua vyema mpinzani wake Florent Ibenge.

Gomez ambaye atakiongoza kikosi cha Simba SC kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika tangu alipoajiriwa kama kocha mkuu mwezi uliopita, amesema anamfahamu vyema Ibenge kuwa ni kocha mzuri na anayependa ‘fair’ lakini hata hivyo yeye anajiamini kutokana na aina ya kikosi alicho nacho.

“Namjua vizuri kocha wao Ibenge, ni mtu mwema, ambaye amekuwa na fair ukikutana nae pia yuko safi lakini hata hivyo kwangu mimi ninajiamini zaidi kwenye mechi hii.”

“Tumefanya maandalizi mazuri ya mechi hii na nimewaambia baadhi ya makosa kwenye mazoezi yetu lakini nimewasisitiza zaidi kwenye suala la kufunga hata kwenye nafasi moja tu kwani hatuwezi kupata nafasi nyingi,” amesema Gomes.

Simba SC iliwasili mjini Kinshasa, Dr Congo tayari kwa mchezo dhidi ya AS Vita Club, ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Tanzania.

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana msimu wa 2018/19 jijini Dar es salaam, Simba SC ilishinda kwa mabao 2-1 na kutinga robo fainali ambayo walifungwa na TP Mazembe kwa mabao 4-1.

TANZIA: Mbunge Nditiye afariki dunia
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Februari 12, 2021