Daktari wa Klabu ya Reims inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa, Bernard Gonzalez (60) amejinyonga baada ya kukutwa na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.

Daktari huyo ambaye amedumu na klabu hiyo kwa miaka 23, alikuwa amejitenga mara baada ya kupata maambukizi na taarifa za kifo chake zimethibitishwa na uongozi wa klabu hiyo.

Ufaransa ni moja kati ya mataifa yaliyoathirika zaidi na ugonjwa huo, ambapo hadi sasa kumesharipotiwa waathirika 92,839, vifo 8,078 huku waathirika 16,183 wakipona kabisa.

Michezo yote nchini humo imesimama, ambapo mamlaka za soka zimesema huenda ligi kuu ikarejea katikati ya mwezi Juni mwaka huu na kusisitiza kuwa ni lazima ligi imalizike kwa gharama yoyote hata kama itakuwa mwezi Julai au Agosti.

Kwa sasa inakadiriwa kuwa vilabu vya soka nchini humo vinapoteza takribani Euro milioni 250 (Tsh. Bilioni 624.5) kwa mwezi kutokana na ligi kusimama.

Waziri mkuu wa Uingereza alazwa akionesha dalili za Corona
Mmarekani aliyekwepa karantini akamatwa Dodoma