Rais wa klabu ya SSC Napoli, Aurelio de Laurentiis amefungua milango ya kumuuza mshambuliaji wake kutoka nchini Argentina Gonzalo Gerardo Higuaín.

Hatua ya rais wa SSC Napoli imekua baada ya kelele nyingi kusikika kwa kudai kwamba, mshambuliaji huyo atakua radhi kuondoka mwishoni mwa msimu huu, baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa muda wa miaka mitatu sasa.

Klabu za nchini England zinatajwa kuwa katika mawindo makali ya kumsajili Higuain kwa lengo la kuviboresha vikosi vyao kwa msimu ujao wa ligi ambao unatabiriwa kuwa ushindani wa haja.

Klabu za Manchester United pamoja na Chelsea zote za nchini England na PSG ya nchini Ufaransa zimekuwa zakwanza kuonekana katika mbio hizo, lakini bado inatajwa zipo nyingine ambazo zitaingia kwenye vita ya kumuwania mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28.

Rais wa klabu ya SSC Napoli, Aurelio de Laurentiis akiwa na Gonzalo Gerardo Higuaín katika sherehe za  utambulisho mwaka 2013

“Endapo ofa nzuri itatufikia na kuturidhisha tutakua na kila sababu ya kumuachia Higuain aondoke.

“Lakini tutazingatia vigezo tunavyovihitaji, ambapo moja ya vigezo hivyo ni nafasi ya klabu itakayoonyesha nia ya dhati, kutokana na muhusika kuhitahi kucheza michuano mikubwa ya barani Ulaya msimu ujao.” Amesema De Laurentiis

Hata hivyo De Laurentiis hakutaja thamani ya mshambuliaji huyo ambaye alijiunga na SSC Napoli akitokea kwa magwiji wa soka wa mjini Madrid nchini Hispania Real Madrid.

Huguain alijiunga na SSC Napoli kwa ada ya uhamisho wa Euro million 40 na mpaka sasa ameshaitumikia klabu hiyo ya mjini Naples katika michezo 102 na kufunga mabao 65.

Man Utd Kumaliza Hesabu Za Renato Júnior Luz Sanches Mapema
Rais Magufuli amtimua Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, kwa kutochukua mshahara wake tangu 2013