Uongozi wa klabu ya Chelsea unajianda kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Argentina na klabu bingwa Italia Juventus Gonzalo Gerardo Higuaín, kwa ada ya Euro milioni 60.

Chelsea wanajipanga kufanya biashara hiyo, kufuatia pendekezo la awali lililotolewa na meneja wao mpya Maurizio Sarri, ambaye mwishoni mwa juma lililopita alitangazwa kumrithi Antonio Conte.

Sarri anaamini kusajiliwa kwa mshambuliaji huyo, kutatoa nafasi kwa Chelsea kumaliza tatizo la ubutu kwenye safu ya ushambuliaji, ambalo lilikua sehemu ya matatatizo yaliyowapa wakati mgumu kutetea ubingwa wa England msimu uliopita.

Meneja huyo kutoka nchini Italia, aliwahi kufanya kazi na Higuain alipokua SSC Napoli, kabla ya kuhamia Juventus mwaka 2016.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini Italia na England vimeripoti kuwa, huenda biashara ya usajili wa Higuaín ikafanyika juma hili, na inatajwa mshambuliaji huyo atasaini mkataba wa miaka mitatu ambao utamuwezesha kulipwa Euro milioni 7.5 kwa mwaka.

Video: Wema Sepetu awaomba watanzania wamuombea
Varane, Modric, Kovacic wapongezwa