Mshambuliaji wa klabu bingwa nchini Italia Juventus FC, Gonzalo Higuain amemfananisha Paulo Dybala na nyota wa Barcelona ambaye ni mshindi mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia “Ballon d’Or” Lionel Messi.

Tangu mwaka jana Dybala alipowasili Juventus akitokea katika timu ya Pelermo kwa haraka staa huyo amewezakuonyesha makali yake na kuisaidia timu hiyo kutwaa mataji ya serea A, Copa Italia na Super Copa Italiana.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, raia wa Argentina pia msimu huu ameendelea na moto huo baada ya kufunga mabao matatu na kutoa pasi zilizozaa mengine mawili na kuifanya Juve kukaa kileleni mwa Ligi hiyo ya serea A wakiwa mbele kwa pointi nne.

Kiwango hicho ndicho kinachoonekana kumkuna raia mwenzake, Higuain ambaye anaamini Dybala ataweza kufuata nyayo za nahodha wa Argentina, Messi.

“Dybala na Messi wana mambo mengi yanayofanana. Messi ni bora na amekuwa akionyesha hivyo kila siku,” alisema Higuain kuuambia mtandao wa Premium Sport.

“Paulo bado ni mdogo kwani ana miaka 23 ila itategemea na kitakachojitokeza siku za mbeleni ila ana kila dalili za kuwa mchezaji bora,” aliongeza staa huyo.

Simba Watamba Kuendeleza Dozi
Cheka Awajibu TPBC, Asema Adhabu Inawahusu Wenyewe