Mshambuliaji kutoka nchini Argentina, Gonzalo Higuain, huenda akabadili upepo wa kucheza soka lake jijini London msimu ujao, baada ya kuonyesha nia thabit ya kuelekea mjini Liverpool.

Higuain, amekua katika mipango ya kutaka kusajiliwa na klabu ya Chelsea chini ya utawala wa meneja mpya Antonio Conte, lakini dalili znaonyesha huenda mambo yakageuka kutokana na mshambuliaji huyo kuweka mkakati wa kujiunga na majogoo wa jiji Liverpool.

Higuian ambaye tayari ameshawekwa sokoni na uongozi wa klabu ya SSC Napoli, ameripotiwa kuwa katika harakati za kulazimisha kusajiliwa na klabu ya Liverpool kutokana na kupendezwa na huduma ya meneja Jurgen Klopp.

Mara kadhaa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, anadaiwa kuweka hadharani mpango huo kwa kuwaambia rafiki zake wa karibu, kwa kusisitiza kutaka kucheza chini ya utawala wa meneja huyo kutoka nchini Ujerumani.

Hata hivyo Klopp atahitaji kufanya usajili wa mshambuliaji wakati wa majira ya kiangazi, kutokana na kumuweka pembeni mshambuliaji aliyemkuta klabuni hapo Christian Benteke, kwa kuona haendani na mfumo anaoutumia tangu alipokabidhiwa benchi la ufundi la Anfield.

Mbali na klabu ya Chelsea kuonyesha nia ya kutaka kumsajili Higuain, klabu nyingine zinazotajwa kuwa katika hatua ya kumsajili ni Manchester United na Arsenal.

Msimu wa 2015-16, Higuain alifanikiwa kufunga mabao 36 katika michezo 35 ya ligi ya Serie A aliyocheza, hatua ambayo ilimuwezesha kushika nafasi ya pili kwenye orodha ya ufungaji bora  nchini Italia.

Kipre Herman Tchetche Aichoka Ligi Ya Bongo
Kocha Wa Uturuki Amtuhumu Luis Enrique Na Watu Wake Wa Barca