Aliyekuwa muamuzi mashuhuri katika ligi ya nchini England pamoja na kwingineko barani Ulaya, Graham Poll, amepingana na wadau wa soka wanaolibeza bao la mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Arsenal Olivier Giroud alilolifunga usiku wa kuamkia hii leo wakati wa mchezo dhidi ya FC Bayern Munich.

Poll, alipingana na wadau wa soka waliokua wanalibeza bao la Giroud, alipokua akichambua maamuzi ya muamuzi kutoka nchini Uturuki, Cüneyt Çakir, aliyechezesha mchezo huo ambao ulikua unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi duniani kote.

Poll, amesema bao la Giroud lilikua halali, japo alionekana amefunga kwa mkono, kutokana purukushani zilizokua zimejitokeza katika lango la FC Bayern Munich wakati wa mpira wa adhabu ulipopigwa na Santi Cazorla.

Amesema dhamira ya Giroud haikuonyesha kama alihitaji kuushika mpira kwa kumuhadaa muamuzi Cüneyt Çakir, bali kilichotokea ni kama bahati mbaya ambayo wakati mwingine imekua ikichukulia kama changamoto kwa waamuzi wengi dunaini.

Muamuzi huyo ambaye alistaafu 2007, ameongeza kwamba Giroud alionyesha nia ya kuupiga mpira uliozaa bao la kwanza la Arsenal kwa kichwa, lakini kutokana na hali ya kusukumana iliyojitokza langoni kwa wapinzani wake, ilisababisha yaliyotokea na kuonekana na wengi ulimwenguni kote.

Katika hatua nyingine Poll, ameshangazwa na wadau wa soka wanaopinga bao la pili la Arsenal lililofungwa na kiungo kutoka nchini Ujerumani, Mesut Ozil katika dakika ya 90 ya mchezo huo.

Amesema bao hilo ni halali na halipaswi kupingwa, kutokana na mpira uliopigwa na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, kuvuka mstari na kuthibitishwa na muamuzi wa pembeni ambaye hufuatilia yanayojiri katika lango la timu husika.

Platini Bado Ana Ndoto Za Kuwa Rais Wa FIFA
Mvuto wa Sura na Umbo wachangia Kuwapa Ushindi Wapinzani, Licha Ya Tafiti Kutowapa Ushindi