Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria Damini Ogulu maarufu Burna Boy, ambaye ameshiriki na kushinda tuzo ya Grammy ya 63 katika albamu yake ya Twice As Tall iliyofanyika mjini Los Angeles.

Tuzo za Grammy zimeielezea albamu ya Twice As Tall kuwa na muziki uliotengenezwa kwa kiwango cha juu cha kimataifa.

Albumu yake ilishirikisha wanamuziki wengi duniani wakiwemo Stormzy, Youssou Ndour, Naughty By Nature, na Chris Martin wa Coldplay, na vilevile Sean Combs akiwa muandaaji mkuu.

Burna Boy amechaguliwa katika kipengele kilekile cha mwaka 2019 – kinachojulikana kama ‘Best World Music Album’ ambapo Angelique Kidjo aishinda katika tuzo za mwaka 2020.

“Burna Boy ni miongoni mwa wasanii wachanga ambao wanatoka Afrika ambao wanabadili mtazamo wa muziki wa Afrika.”amesema Kidjo

Itakumbukwa Burna Boy alizindua albamu yake ya kwanza ya LIFE, mwaka 2013. Na baadae alizindua albamu ya Redemption mwaka 2015 na Outside mwaka 2018 ambayo ilijumuisha ngoma iliyovuma kimataifa ya Ye.

Katika albamu yake ya mwaka 2019 ya African Giant, Burna Boy alijulikana zaidi kimataifa na kupata tuzo yake ya kwanza ya Grammys.

.

Velud aikana Young Africans
Hitimana na mkakati wa kuinusuru Mtibwa Sugar