Mshambuliaji Antoine Griezmann amesisitiza suala la kutaka kuendelea kufanya kazi na meneja wa Atletico Madrid, Diego Simeone ambaye ameanza kutajwa huenda akaondoka Vicente Calderón Stadium kipindi kifupi kijacho.

Griezmann ambaye amekua mshambuliaji hatari tangu alipojiunga na Atletico Madrid mwaka 2014 akitokea Real Sociedad, amesema Simione amekua nguzo kubwa katika mafanikio ya klabu hiyo ambayo inatoa upinzani mkali kwa magwiji wa La Liga (FC Barcelona na Real Madrid).

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, amesema haoni sababu za Simione kuhusishwa na mipango ya kutaka kuondoka klabuni hapo, ambapo anahisi ndio mahala sahihi kwake, kutokana na ukomavu wa kikosi alichokijenga kwa mikono yake.

“Nimekua na furaha wakati wote tangu nilipohamia Atletico Madrid, na hii inatokana na uhusiano wa karibu uliopo kati yangu na Diego Simione ambaye amekua mkarimu kwa kila mmoja wetu,”

“Uwepo wa Simeone umenifanya nijifunze mambo mengi sana katika soka la ushindani na ninamini kinachozungumzwa na kama itatokea basi hata mimi huenda nikafanya jambo tofauti.”

“Nimekua ninaogopeshwa sana na kauli yakuondoka kwa Simeone japo wakati mwingine ninaipuuzia – ninahitaji kuendelea kujifunza mengine kutoka kwake.” Griezmann alikiambia kituo cha radio cha Onda Cero.

Hii inakua ni mara ya pili kwa Diego Simione kuhusishwana mipango ya kutaka kuachana na klabu ya Atletico Madrid, kwani kama itakumbukwa vyema, mwishoni mwa msimu uliopita jambo hili lilizungumzwa katika baadhi ya vyombo vya habari na klabu zilizotajwa kuhitaji huduma yake zilikua Chelsea, Man United pamoja na Paris Saint-Germain.

Mtoto: Natamani ningekuwa smart phone
Majaliwa azindua mfumo wa tiketi za kielektroniki kuingia uwanja wa Taifa