Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann amesema tayari amefanya maamuzi juu ya klabu atakayoichezea msimu ujao.

Griezmann ambaye amefunga jumla ya mabao 29 katika michezo 49 aliyoichezea Atletico Madrid msimu uliopita amekuwa akiwindwa kwa karibu na vilabu vya Manchester United na Barcelona.

Akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa jana jumanne alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alisema tayari anajua hatma yake msimu ujao lakini hakutaja ni klabu gani atakwenda.

”tayali nimefanya maamuzi juu ya mustakabari wangu lakini leo sitoeleza juu ya hili kwakuwa sio wakati na sehemu sahihi” alisema Griezmann.

Mshambuliajii huyo ni mmoja kati ya wachezaji tegemezi wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kitakachoshiriki michuano ya kombe la Dunia inayotarajia kuanza kutimua vumbi kesho nchini Urusi.

 

Nchemba afafanua kuhusu haki ya mtuhumiwa
TCRA yatoa mbinu kukabiliana na wezi wanaotoa namba ya simu kutumiwa pesa

Comments

comments