Na Gift Macha

Baada ya Manji kuondoka Yanga, hali ilikuwa mbaya sana.. Yanga haikuwa na uwezo wa kusajili wachezaji wa maana.. Haikuwa na uwezo wa kuweka kambi nzuri wala kusafiri vizuri kwenda mikoani.. Hali ilikuwa mbaya kweli kweli.

Hata hivyo baada ya kuja GSM mambo yamebadilika sana.. Haya ni maeneo ambayo GSM wamewekeza msimu huu.

1. Usajili

Wachezaji wote wanaotamba Yanga msimu huu wameletwa na nguvu ya GSM. Tazama mabeki Kibwana Shomary, Yassin Mustapha, Bakari Mwamnyeto, Dickson job. Viungo Mukoko Tonombe, Feisal Salim ameongezewa mkataba na GSM. Kina Tuisila Kisinda, Saido Ntibazonkiza na Yacouba Sogne pia ni matunda ya GSM.

Bahati mbaya ni kwamba wachezaji wengine waliosajiliwa kwa mategemeo makubwa kama Michael Sarpong, Waziri Junior, Fiston Abdoul Razack na wengineo wamewaangusha GSM.

2. Makocha

Yanga msimu huu imekuwa chini ya makocha watatu wa kigeni na wote wameletwa na GSM. Alianza Zlatko Krmpotic, Cedric Kaze na sasa Mohammed Nabi. Zlatko na Kaze wamewaangusha sana GSM.. Hasa Kaze ambaye aliaminiwa zaidi.. Na dhambi kubwa itakayomtafuna Kaze ni kuwaletea Fiston. GSM pia imeleta kocha wa viungo, makipa na wengineo.

3. Kambi ya Kisasa

Wachezaji wa Yanga wapewe nini tena? Wanaishi kisasa mno pale Avic Town Kigamboni.. Eneo la kitajiri. Kambi imetulia kinoma.. Wanaishi vizuri kweli kweli.. Hii ni nguvu ya GSM. Kama unakataa uliza gharama za kuishi pale kwa mwezi mmoja zikoje..

4. Usafiri wa anga, hotel za kisasa

Yanga siku hizi inapaa juu kwa juu kwenda mikoani.. Zile safari za basi zimebaki historia.. Na kila wakisafiri kwenda mkoani wanakaa hoteli za kisasa zaidi.. Inavutia sana.. Bahati mbaya ni kwamba pamoja na yote haya, wachezaji bado hawajajituma vya kutosha kuhakikisha wanashinda mechi nyingi za ugenini.

Hata hivyo pamoja na yote, nani aliwaza Yanga ingeweza kuongoza Ligi kwa kipindi kirefu msimu huu? Hakuna. Ila GSM wamefanya hilo liwezekane.

Yanga ya msimu huu ni imara zaidi ya zile za misimu miwili nyuma.. Yanga hii inaonyesha mwanga na huenda ikatikisa miaka miwili ijayo kama uwezekazaji wa GSM utaendelea.

Bila shaka tunahitaji kutambua huu mchango wa GSM kwa Yanga..

Zebaki inavyoathiri maisha ya wachimbaji Tanzania
ASFC: KMC FC yaiwinda Dodoma Jiji FC