Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola ameeleza umuhimu wa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chelsea walioupata mwishoni mwa juma lililopita kwenye Uwanja wa Etihad.

Guardiola amesema ushindi huo ni muhimu kwa Manchester City, lakini akasisitiza kuwa taji la Ligi Kuu England bado sana na katu taji hilo huwezi kutwaa mwezi Januari.

Guardiola amesema: “Ushindi muhimu kwa sababu tunacheza dhidi ya mshindani mkubwa,”

“Unapopata pointi tatu, hawawezi kupata pointi tatu na ni wiki moja pungufu.”

“Lakini Januari hakuna bingwa. Tunaweza kufikiria kuhusu Chelsea, na Liverpool wana mechi mkononi. Wakishinda itakuwa na pointi nane na pointi nane Januari si kitu.

“Nataka kushinda endapo tunastahili, na tulistahili. Ninapenda soka kuwa la haki kwa hiyo, wakati nilikuwa na furaha kushinda dhidi ya Arsenal, hatukustahili. Kushinda wakati unastahili hujisikia vizuri.”

Manchester City inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa kufikisha alama 56, ikifuatiwa na Liverpool yenye alama 45 huku Chelsea ikiwa nafasi ya tatu kwa kumiliki alama 43.

Watu 22 wafariki kwa tetemeko la Ardhi
Martial akanusha tuhuma Man Utd