Meneja wa klabu bingwa nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Pep Guardiola amesema yupo njiapanda huku akiendelea kutafakari msimu ujao ataifundisha timu gani.

Akizungumza na baadhi vyombo vya hbari, alisema hivi sasa amepokea ofa za timu nyingi kwa ajili ya kutaka kuzinoa.

Alisema bado anaendelea kuwasiliana na familia yake, wakala wake na jamaa zake wa karibu kwa ajili ya kujua hatima yake msimu ujao.

“Najaribu kuangalia uwezekano nini cha kufanya kabla ya kutoa maamuzi, lakini kazi hiyo ninaifanya kwa kuwashirikisha watu mbalimbali,” alisema.

Hata hivyo kocha huyo ameonyesha nia ya kutaka kutua nchini Uingereza ambapo wakala wake amekuwa anafanya vikao na baadhi ya viongozi wa timu za nchi hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya kocha huyo kugoma kuongeza mkataba wa kuendelea kuinoa Bayern katika msimu ujao.

Mwigulu Nchemba asimamisha watumishi wengine na kuvunja bodi
Ufalme Wa Soka La England Wapelekwa Emirates Stadium