Baada ya kuambulia kisago cha mabao mawili kwa sifuri kutoka kwa Arsenal, meneja wa klabu bingwa nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Pep Guardiola amekataa kumlaumu mlinda mlango Manuel Neuer kufuatia kuonekana kuwa chanzo cha kupoteza mchezo huo.

Guardiola, amekataa kuelekeza lawama kwa mlinda mlango huyo mashuhuri ulimwenguni kote, kutokana na wachambuzi wa soka pamoja na waandishi wa habari kuona Neuer alishindwa kuonyesha ubora wake katika mchezo huo.

Neuer, anadaiwa kufanya makosa makubwa na kusababisha bao la kwanza lililofungwa na mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Olivier Giroud, kufuatia mpira wa adhabu uliokua umepigwa na kiungo kutoka nchini Hispania Santi Cazorla katika dakika ya 77.

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 29 alionekana kutoka golini na kuufuata mpira huo, bila mafanikio na hatimae kujikuta akitoa mwanya kwa Giroud kufunga kwa urahisi bao lililoipa Arsenal nafasi ya kuongoza katika mchezo huo, kabla ya kiungo kutoka nchini Ujerumani Mesut Ozil hajaongeza bao la pili katika dakika ya 90.

Guardiola aliwaambia waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo, kikosi chake kwa ujumla hakikikucheza vyema, hivyo hana budi kukiri mapungufu hayo, lakini si kumtazama mchezaji mmoja ambaye ameonekana kunyooshewa vidole na walio wengi.

Amesema katika maisha yake hakuwahi, kumlaumu mchezaji mmoja kwa kisingizio cha kupoteza mchezo, zaidi ya kuamini umoja na mshikamano wa timu ndio chanzo cha kupoteza ama kupata mafanikio.

Kwa ushindi huo Arsenal, amejikusanyia point tatu za mwanzo katika michezo ya kundi la sita, baada ya kusota kwenye michezo miwili iliyopita kwa kukubali kufungwa na Dynamo Zagreb pamoja na Olimpiakos.

Mourinho Ajiweka Kikaangoni UEFA
Mwisho Wa Ubaya Aibu, Madudu Yabainika FIFA