Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Ally Gugu amewapongeza wafanyabiashara kwa kujumuika pamoja katika kuwasilisha changamoto zilizopo ndani ya masoko na kuweka kwa pamoja mikakati ya ufumbuzi na amewasisitiza kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu.

Gugu ameyasema hayo katika kikao cha Wafanyabiashara na kuongeza kuwa, “Serikali itahakikisha eneo letu la Makao Makuu ni sehemu sahihi na wezeshi kwa wafanyabiashara lazima kuwa na mahali sahihi pakufanya biashara eneo ambalo halitakuwa na changamoto ili biashara ziweze kushamiri na kuweza kupata faida ninyi kwa mmoja mmoja na Serikali kwa ujumla.”

Kikao hicho, kiliazimia maazimio ambayo yataboresha biashara zao ikiwa ni  pamoja na Halmashauri
kuchukua hatua madhubuti kwa wanaomiliki vizimba na kutofanya biashara, kuundwa kwa timu itakayopitia Sheria ya kodi ili  kuunganisha Serikali na sekta binafsi na kuundwa kwa kamati ya utatuzi
wa changamoto za masoko kama ilivyokuwa kwa soko la Machinga.

Maazimio mengine yaliyokubalika ni pamoja na kuwepo kwa taasisi moja ya kukusanya tozo, Jiji kukamilisha miundombinu kwenye baadhi ya masoko na kutoa elimu kwa umma hasa Wafanyabiashara kuhusu matumizi ya mfumo wa TAUSI.

Siku ya Mazingira: GGML yatoa elimu taka za plastiki
Wanajeshi wawili wafariki kwa ajali ya Helikopta