Diamond Platnumz na Wema Sepetu ambao mapenzi yao yanatajwa kuwa ni ‘Zilipendwa’, wamezua gumzo mitandaoni baada ya kuonekana jana wakiwa katika ukaribu wa ‘kupetipeti’ hadharani.

Wawili hao ambao walikutana wikendi hii kwenye hafla iliyoandaliwa na WCB ya kumpokea mwimbaji Mbosso kwenye timu hiyo iliyofanyika katika hotel moja kubwa jijini Dar es Salaam, walizungumza kwa ukaribu, nyuso zao zikisogeleana mithiri ya kinda na mama wanaotaka kulishana chakula.

Kikubwa kilichozua gumzo lingine katika dakika chache ni hatua ya Diamond kumtuliza Wema kifuani kwa sekunde kadhaa na kisha kumnong’oneza huku wakielewa wazi kuwa mapaparazi walikuwa wakiendelea na kazi mbele yao.

Ingawa haijafahamika walizungumza nini wakati huo, Diamond amewahi kueleza hivi karibuni kuwa bado ana urafiki wa karibu na Wema na wamekuwa wakisapotiana kwenye masuala ya biashara na maisha kwa ujumla.

Hata hivyo, hatua hiyo ya wawili hao huenda ikageuka kuwa mwiba mwingine kwa mama watoto wa Diamond, mrembo kutoka Uganda, Zari.

Timu za mitandaoni za wawili hao zimeendelea kuwekana kitimoto kuhusu kilichojiri.
Video kwa hisani ya mtandao wa Dizzimonline.

Polepole aibua mapya shambulio la Lissu kupigwa risasi
Arsenal yakaribia kumnasa Aubameyang