Meneja wa muda wa klabu ya Chelsea,  Guss Hiddink anafanya kazi ya kipekee tangu alipokabidhiwa  mikoba ya  Jose Mourinho aliyetimuliwa mwishoni mwa mwaka jana.

Wakati Mourinho anaondoka tayari klabu hiyo ilikuwa imeshapoteza michezo tisa kati ya kumi na sita ya ligi kuu ya soka nchini England.

Rekodi hazidanganyi kutokana na klabu ya Chelsea kutofungwa mchezo hata mmoja tangu Jose Mourinho alipoondoka Klabuni hapo.

Chelsea wamefanikiwa kushinda michezo miwili na kusuluhu mingine sita katika jumla ya michezo nane waliyocheza tangu kutimka kwa “The Special One”

Ikiwa Chelsea wataendelea na kiwango hiki walichonacho basi wanaweza kupunguza pengo la pointi lililopo kati yake na timu zilizopo nusu ya msimamo wa Ligi kuu England japokuwa si rahisi kwa sasa kusema kuwa klabu hiyo inaweza kukwea mpaka nafasi ya 4 lakini matumaini yapo kuwa wanaweza kutoka pale walipo kwa sasa.

Michezo inayofuata ni Chelsea dhidi ya Manchester United itakayopigwa Jumapili ya Februari 7 katika uwanja wa Stamford Bridge uwanja ambao kwa misimu miwili mfululizo Manchester United wamepokea kichapo kikiwepo kile cha goli 3-1 kutokana na Hat trick ya mkameruni Samuel Eto’o Fills.

Mayanja Awajibu Wanaomtaka Said Demla Kikosini
Ligi Daraja la pili Nayo Kuchanja Mbuga Wikiendi Hii