Meneja wa muda wa klabu ya Chelsea, Guus Hiddink amesema kabla ya Leicester City kumchukua Claudio Ranieri ilimwomba awe meneja wa klabu hiyo ambayo imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza 2015/2016.

Hiddink alisema kipindi ambacho Leicester walimuomba kuwa meneja wa klabu hiyo, alikataa kutokana na kuhitaji kumpumzika hivyo alikataa na baadae wakamchukua Ranieri.

“Ni kweli Leicester waliniomba kuwa kocha wao kwa msimu huu, lakini niliwambia nahitaji kumpuzika na sihitaji kufanya chochote,” Hiddink aliiambia Telesport.

Aidha meneja huyo kutoka nchini Uholanzi, aliongeza kuwa baada ya sare na Tottenham, kocha wa Leicester City, Claudio Ranieri alimpigia simu na kumshukuru kwa kuwazuia Tottenham na kuiwezesha Leicester City kushinda ubingwa wa EPL 2015/2016.

Ni Real Madrid Vs Atletico Madrid Fainali Ya Ligi Ya Mabingwa Ulaya
Picha: Daladala yaacha njia na kugonga basi la mwendo kasi