Aliyekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uholanzi Guus Hiddink anakaribia kuteuliwa kaimu meneja wa Chelsea baada ya Jose Mourinho kufutwa kazi.

Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 69 kwa sasa yumo mazungumzoni na wawakilishi wa Chelsea katika hoteli moja London.

Hiddink, aliwahi kunoa Chelsea wakati mmoja, alipowasaidia kushinda Kombe la FA mwaka 2009, lakini bado hajatia saini mkataba.

The Blues wamo nambari 16 ligini kwa sasa baada ya kushindwa mechi tisa kati ya 16 walizocheza msimu huu Ligi Kuu Uingereza.Mourinho alifutwa kazi Alhamisi, miezi saba pekee baada ya kuwaongoza Chelsea kutwaa ubingwa wa Ligi ya Premia.

Hiddink alishinda mataji sita ya ligi ya Uholanzi na Kombe la Ulaya akiwa meneja wa PSV Eindhoven ya Uholanzi katika vipindi viwili.

Pia aliongoza timu za taifa za Korea Kusini, Australia na Urusi kabla ya kujiunga na Chelsea mara ya kwanza kujaza pengo lililoachwa na Luiz Felipe Scolari Februari 2009.

Alijiuzulu wadhifa wake kama mkufunzi wa timu ya Taifa ya Uholanzi mwezi Juni, baada ya kutofanya vyema katika juhudi za kuwasaidia kufuzu kwa Euro 2016.

Azam FC Wawafuata Majimaji Mkoani Ruvuma
Blatter Akiri Kuhisi Machungu Ya Adhabu Ya FIFA