eshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, jana lilimkamata Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, alipotua akitoke nchini Kenya.

Gwajima amekuwa akisakwa na jeshi hilo tangu katikati ya mwezi Juni alipotoa kauli tata akimkosoa Rais mstaafu, Dk. Jakaya Kiwete na kumshauri Rais John Magufuli kuihama CCM endapo kile alichodai mbinu alizonasa za kutaka kutomkabidhi uwenyekiti wa chama hicho zitaanza kuibuliwa.

Taarifa za kuaminika zimeeleza kuwa Gwajima alikuwa akisubiriwa na helicopter yake ili aweze kuelekea katika hotel ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko baada ya safari hiyo, lakini makachero wa polisi waliokuwa wakimsubiri walimtia nguvuni na kumfikisha katika kituo cha polisi ambapo alihojiwa kwa saa nne.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alithibitisha kukamatwa kwa Gwajima na kuhojiwa, na kwamba aliachiwa siku hiyohiyo kwa dhamana.

“Ameletwa, amehojiwa na amepewa dhamana. Uchunguzi unaendelea,” alisema Kamanda Sirro.

Vyanzo vimedai kuwa Jeshi hilo linazishikilia simu za kiganjani za Askofu huyo kwa ajili ya uchunguzi.

Carlo Ancelotti Asisitiza Kuondoka Kwa Mario Gotze
Rashid Mandawa,Cassian Ponera Wasajiliwa Mtibwa Sugar