Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima, Gwajima ameitisha vyombo vya habari kuzungumzia sakata lake la video iliyosambaa akiwa faragha.

Fuatilia kupitia mitandao yetu ya kijamii tutakuwekea mubashara yote yatakayojiri kanisani kwake ambapo vyombo vya habari vimekusanyika kumsikiliza.

Mapema jana Kamanda Mambosasa amemtaka Askofu Gwajima kuripoti polisi leo majira ya saa nne au saa tano kufuatia kusambaa kwenye mitandao ya kijamii video yake akiwa faragha.

Mambosasa amesema Gwajima amekiuka maadili hivyo ametakiwa kuripoti polisi kutoa maelezo zaidi.

Hadi sasa Ubungo kanisani kwake vyombo mbalimbali vya habari vimeitikia wito huo.

Fuatilia moja kwa moja toka instagram ya Dar24 tumekuwekea mubashara yanayojiri kanisani hapo.

Aidha ifahamike kuwa suala hili limemgusa kila mtu kwa namna yake ukizingatia wadhifa mkubwa alionao mchungaji Gwajima wa kuwaongoza waumini wengi ambao wanamwamini na kumfuata katika kanisa la Ufufuo na uzima.

video: Asimulia walivyopewa mtaji na Dk. Mengi mwaka 1995
Habari picha: Hali inayoendendelea Dar kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha

Comments

comments