Leo askofu Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima amezungumza na vyombo vya habari kufuatia sakata la kusambaa kwa video zikidai kuwa yupo faragha na mwanamke ambaye bado hajafahamika.

Gwajima amesema aliyeoneka kwenye video hiyo sio yeye bali ni picha za mtu mwingine zimeungwaungwa na kuonesha kama yeye.

”Amethibitisha kuwa mimi ni mwanaume, nimekaa vizuri isipokuwa kuwa tu sasa angeniweka mimi mwenyewe, kuliko kuunganisha unachukua mwili wa mtu unachomeka kichwa unafanya hivi, kulikuwa na watu ambao wapo hapa wamesema wacha tueleze tekniki ya video iliyofanyika nikawaambia haina haja ya kuelezea” Amesema Gwajima.

Ameongezea kuwa video hizo aliziona jana asubuhi ila hakutaka kuongea na kuamua kufanya uchunguzi ajue mtu aliye nyuma yake.

”Hata kama tukio hili lingekuwa ni kweli aliyerusha  nia yake sio nzuri, anajua mimi nina mke na watoto wakubwa na nina makanisa zaidi ya 400. Lengo la mtu huyu haliwezi kuwa zuri ni zaidi ya kunichafua ni lengo la kishetani” amesema Gwajima.

Ameongezea Safari hii itakuwa kali kuliko ile ya zamani na amesema mtajua Mungu yupo.

”Ninaomba mjiulize hivi ni mwanaume gani anaweza kujirekodi halafu atume mwenyewe na ule mkono ni wa baunsa” amehoji Gwajima.

Naye mke wa Gwajima amepata nafasi ya kuongea mbele ya vyombo vya habari kuhusu sakata hilo amesema kuwa anamuamini sana mume wake na anaamini hawezi kufanya tukio hilo lililosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha Askofu Gwajima amesema atalifuatilia suala hil na kujua nani yupo nyuma ya tukio hili la kumchafua na ameahidi kuendelea kutoa taarifa zaidi kwa kitakachoendelea katika sakata hili.

 

LIVE: MWILI WA DKT. MENGI UKIWASILI KILIMANJARO MUDA HUU
video: Asimulia walivyopewa mtaji na Dk. Mengi mwaka 1995

Comments

comments