Wabunge Josephat Gwajima Kawe na Jerry Silaa Ukonga ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge wameondolewa kwenye kamati hiyo hadi itakapoamuliwa vinginevyo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti Emmanuel Mwakasaka, kamati hiyo ina jumla ya wajumbe 24 wakiwamo Gwajima na Silaa na sasa imebaki na wajumbe 22.

“Unapotuhumiwa mara nyingi, wewe ndio mshtakiwa zipo taratibu zinafuata. Kama wewe ni mtuhumiwa huwezi kuwa hakimu kwenye kesi yako mwenyewe,” amesema Mwakasaka .

Itakumbukwa Jumamosi wiki iliyopita Spika Ndugai aliamuru Gwajima na Silaa wapelekwe kwenye kamati hiyo, ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

Gwajima alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo jana wakati Silaa atatakiwa kufika kwenye kamati hiyo leo saa 7.00 mchana.

Kenyatta amemtaka Ruto Kujiudhulu
Rais Samia kuhudhuria uapisho wa Rais wa Zambia