Raia wa Uswizi na Italia, Gianni Infantino ameshinda kinyanyiro cha kuwania urais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), hivyo kutangazwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho hilo akichukua nafasi iliyoachwa na Sepp Blatter.

Infantino mwenye umri wa miaka 46 ameshinda uchaguzi huo kwa kupata kura 115 akimzidi mshindani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa kwa kura 27.

Prince Ali bin al-Hussein aliyeshika nafasi ya tatu akiambulia kura nne pekee, huku hali ikiwa mbaya zaidi kwa Jarome Champagne ambaye hakupata kura hata moja, huku Tokyo Sexwale kutoka Afrika Kusini akijiengua mwenyewe kabla ya zoezi la upigaji kura.

Nafasi hiyo iliachwa wazi na Blatter aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi baada ya kukalia kiti hicho tangu mwaka 1998. Mwaka jana alilazimika kujiuzulu na baadae kufungiwa kushiriki michezo kwa muda wa miaka 8, alikata rufaa na kupunguziwa miaka miwili, hivyo ana pingu za miaka 6 bila kujihusisha na soka.

Infantino alikuwa Katibu Mkuu wa UEFA tangu mwaka 2009.

 

Shabiki amtega Ali Kiba... Ni kama alitaka aangukie kwa Diamond
Coastal Union Yakiangusha Kigogo Kingine