Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imetupilia mbali kesi ya kupinga matokeo yaliyompa Ubunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), iliyofunguliwa na aliyekuwa mpinzani wake kwenye Uchaguzi huo, Frederick Mwakalebela (CCM).

Mahakama hiyo pia imeamuru Mwakalebela kumlipa Mchungaji Msigwa gharama za kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka jana na kupata usajili wa mahakama hiyo Novemba 30.

“Kesi ya mwakalebela yatupwa anatakiwa kulipa gharama. Nikiwa na wakili wangu msomi Jane Masey,” Mchungaji Msigwa ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook akiambatanisha picha yake na Wakili wake.

Katika shauri la msingi la kesi hiyo namba 5 ya mwaka 2015 ya kupinga matoke, Mwakalebela aliwatuhumu Mchungaji Peter Msigwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini, Ahmed Sawa kwa kukiuka sheria na taratibu za uchaguzi hali iliyopelekea yeye kupata matokeo mabaya yasiyo halali.

 

Shilole atangaza kazi ya mwalimu wa kiingereza, Chukua namba yake hapa
Exclusive: MC Pilipili asimulia alivyotafutwa na TRA baada ya kutangaza Ma-MC walipe kodi, Utacheka (Audio)