Mbunge wa Busega Dkt. Raphael Chegeni akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha Rose Migiro mara baada ya kufanya mazungumzo na watanzania wanaoishi na kufanya kazi Uingereza katika fani mbalimbali za afya na biashara.
 
Watanzania hao wamekubali kupitia umoja wao kuunga jitihada za Rais Dkt. John Magufuli katika kusaidia upatikanaji wa vifaa muhimu vya kisasa, kuchangia fedha na watalaam wa afya ili kuboresha huduma za afya nchini.
 
Watanzania hao wamepongeza jitihada za serikali ya awamu ya tano katika ujenzi na uboreshaji wa huduma za afya mijini na vijijini ambapo serikali imekuwa ikijenga Hospitali, vituo vya afya na Zahanati katika kila Kata.

Justin Bieber ampa makavu Eminem
Kim Jong Un ashuhudia majaribio ya makombora, Trump amwandikia ujumbe