Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipokea Gwaride rasmi lililoandaliwa na Vijana wa Chipukizi Tanzania, alipowasili katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita leo Oktoba 14,2021 kwa ajili ya kushiriki katika kilele cha Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru na kumbukizi ya miaka 22 ya kifo cha Baba wa Taifa katika uwanja wa Magufuli Chato.
Gwaride rasmi lililoandaliwa na Vijana wa Chipukizi Tanzania, wakiwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati akipokea Gwaride hilo katika uwanja wa Magufuli wilayani Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipozuru Kaburi hilo leo Oktoba 14, 2021. alipokua njiani akielekea katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita kwa ajili ya kushiriki katika kilele cha mbio maalum cha Mwenge wa Uhuru.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja akitoa sadaka wakati wa misa maalum ya kuwaombea Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Abeid Amani Karume, Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi waliopo madarakani wakiongozwa na Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja (kulia) akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe.Dkt. Stergomena Tax mara baada ya misa maalum ya kuwaombea Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Abeid Amani Karume, Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi waliopo madarakani wakiongozwa na Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
NARCO yaja na suluhu migogoro ya wafugaji
Luis Miquissone: Sitaiacha Simba, ni familia yangu