Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefanya ziara Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Narungombe.

Wairi Mkuu amefanya ziara hiyo hii leo Novemba 18, 2022 ambapo pia amekagua ujenzi wa Kituo cha Afya Nangurugai na kuzungumza na wanawake ambao walikuwa wakipata huduma za matibabu ya watoto wao katika Kituo cha Afya cha Narungombe Wilayani Ruangwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na akina mama waliofika kupata huduma za matibabu ya watoto wao  katika Kituo cha Afya cha Narungombe wilayani Ruangwa hii leo, Novemba 18, 2022. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Frank Chonya (wa tatu kulia), akimpa maelezo Waziri Mkuu kuhusu ujenzi wa Kituo cha Afya cha Namgurugai.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Narungombe hii leo Novemba 18, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya Nangurugai wilayani Ruangwa, hii leo Novemba 18, 2022. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Frank Chonya.

Ndege za Kijeshi zatumika kupambana na waasi
Msaada Bil. 210 utekelezaji miradi mbalimbali