Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Octoba 2, 2021 ameshiriki maadhimisho ya siku ya mlezi wa Skauti Tanzania Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimvisha Tuzo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, kwa kutambua mchango wake katika kuunga mkono Skauti Tanzania, kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania yaliyoadhimishwa leo Oktoba 02, 2021 katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimvisha Tuzo Kamishna Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Salum Hamduni kwa kutambua mchango wake katika kuunga mkono Skauti Tanzania, katika Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania yaliyoadhimishwa leo Oktoba 02, 2021 katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania yaliyoadhimishwa leo Oktoba 02, 2021 katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Kamishna Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Salum Hamduni akimkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mwongozo wa kuwawezesha na kuwafundisha vijana wa Skauti jinsi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini, kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania yaliyoadhimishwa leo Oktoba 02, 2021 katika Viwanja vya Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma.
Vijana wa Skauti wa Mkoa wa Simiyu Penina Mashimo kulia na Anastandhia Limbe kushoto, wakimvisha Skafu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipowasili katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo Oktoba 02, 2021 kwa ajili ya kuhudhuria katika Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania.

Classic Finishes Suluhu gharama za vigae
Watuhumiwa 305 wakamatwa kwa makosa mbalimbali