Rais wa Haiti Jovenel Moise leo ameweka shada la maua katika makumbusho ya mamia kwa maelfu ya watu waliofariki dunia kutokana na tetemeko baya la ardhi lililoikumba nchi hiyo mwaka 2010.

Baada ya kuweka shada hilo Moise amewataka raia wa Haiti kuonyesha umoja na mshikamano kama walivyofanya baada ya tetemeko hilo.

Mnamo Januari mwaka 2010 tetemeko lenye kipimo cha 7.0 liliitikisa Haiti nje kidogo ya Mji Mkuu Port-au-Prince na kuwauwa watu laki tatu hiyo ikiwa ni kulingana na takwimu za serikali.

Zaidi ya watu milioni moja nukta tano wengine waliachwa bila makao na kupelekea mzozo wa kibinadamu katika kisiwa hicho.

Serikali za kigeni na mashirika ya kimataifa yaliahidi misaada ya mabilioni ya dola ingawa wachumi wanakiri kwamba ni kiasi kidogo mno cha fedha kilichowafikia wahanga.

Ufilipino: Hofu yazidi mlipuko wa Volcano
Uwasa yaja na mpango wa mita kujisoma zenyewe