Aliyekuwa mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya Chadema, Haji Duni Haji amezungumzia hatma yake ya kisiasa kama ataendelea kubaki katika chama hicho kwakuwa aliingia Chadema akitokea CUF ili kukidhi vigezo vya kisheria vya kuwa mgombea mwenza wa urais ikiwa ni sehemu ya mpango maalum wa UKAWA.

Mwanasiasa huyo Mkongwe ameeleza kuwa hivi sasa anaendelea na michakato yake ya kisiasa na kwamba ataweka wazi uamuzi wake ifikapo Januari mwakani.

“Kwa sasa sisemi jambo lolote, nitakuambia baadaye kidogo kama nitarudi CUF au nitabakia Chadema. Kuna mambo ninafanya kwanza, nisingependa kusema,” alisema.

Katika hatua nyingine, Haji Duni aliitaka serikali kulinda katiba katika mgogoro wa uchaguzi unaoendelea visiwani Zanzibar. Alisema kuwa kurudiwa kwa uchaguzi visiwani humo kunaweza kusababisha vurugu na kupoteza amani katika visiwa hivyo kama ilivyo nchini Burundi.

Aliitaka serikali kuiangalia Zanzibar na kusaidia kutangazwa kwa mshindi wa uchaguzi uliopita.

Ukawa wamtetea Mkurugenzi wa Kinondoni Aliyesimamishwa, Watoa Nyaraka
Ufisadi: Kigogo Adaiwa Kutumia Fedha Za Umma Kufanya 'Masaji' Na Mrembo Wake