Vita kati ya mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa klabu ya Simba SC Haji Manara dhidi ya wachambuzi wa soka nchini imeendelea kudhihiri, baada ya kuwazungumzia katika mkutano wake na waandishi wa habari alioufanya jana kwenye ukumbi wa makao makuu ya klabu hiyo kongwe hapa nchini.

Haji Manara alisema wachambuzi wa soka nchini wamekua wakifanya kazi zao chini ya kiwango, kwa kuegemea upande mmoja miongoni mwa klabu kongwe hapa nchini na kuisifia Young Africans kila kukicha, huku wakishindwa kufanya upembuzi yakinifu kwa kutumia takwimu (Data).

Manara alisema wachambuzi wa soka nchini wamekua wakiizungumza na kuiandika vibaya klabu ya Simba SC, kwa minajili ya kuishambulia, jambo ambalo aliahidi hatolivumilia na badala yake atasema kwa kuitetea klabu yake ambayo anaitumikia kama mkuu wa idara ya habari na mawasilkno.

Muda mchache uliopita Manara amemjibu mmoja wa wachambuzi aliyeandika makala kuhusu alichokizungumza jana katika mkutano na waandishi wa habari, kwa kuandika makala aliyoipa jina la NI HARAAM KUMUUACHIA MTU HUYU!!

Makala ya Haji Manara imesomeka kama ifuatavyo

NA: HAJI S. MANARA

Salaam

Kiasili Haji Manara sio mtu dhaifu anayeweza kukalia kimya shutuma zinazokuja kwake binafsi au taasisi anayoingoza na kuifanyia kazi, ni aina ya mtu anayejua thamani ya habari, anaetaka na kuamini usahihi wa jambo liliopo na linalokuja kwa kadri lilivyo.

Nimeanza na dokezo hilo kusudi ili tuende sawa kwanza, ili kujibu tuhuma na shutuma zinazoelekezwa na baadhi ya magwiji wa ukosoaji nchini hususan kwenye tasnia yetu hii ya kandanda nchini.

Baada ya mkutano wangu na vyombo vya habari hapo jana j.nne ya tarehe 31-10-2017 pale klabuni Msimbazi, kumetokea wakosoaji wakubwa dhidi yangu binafsi, na wengine wakienda mbali zaidi kwa kunifananisha hata na msemaji wa klabu ya Yanga.

Nianze na hili la maudhui ya mkutano wangu wa jana na wanahabari.

Kwanza niweke wazi kama mtu nnayesimamia idara ya Habari ya klabu, sina mamlaka yoyote ya kuitisha press bila idhini ya uongozi wa klabu ya Simba, na ktk hili simjui yoyote afanyae kazi kama yangu mwenye mamlaka ya kuongea na waandishi bila idhini ya Uongozi wa taasisi anayoifanyia kazi.

Kwa muktadha huo, press yangu ya jana ina baraka zote za uongozi wa Simba SC, na maudhui ya nilichokizungumza jana ni matakwa halali ya uongozi.

Lakini pia niuarifu umma kuwa bado ninaamini pamoja na wanadaamu kutokuwa wakamilifu, waamuzi waliochezesha mchezo wa jmosi dhidi ya Yanga na wale waliochezesha michezo mingine niliyoizungumzia jana, kuna makosa waliyafanya na mm kama msemaji wa klabu, ilikuwa ni wajibu wangu kuzungumzia hilo.

Inawezekana labda kwa baadhi ya watu haikuwa sahihi kwao, lakini dhamira ya klabu ya Simba sio kushutumu, bali ni kutaka ‘fair game’ hatutaki kupendelewa wala kuonewa, na ndio maana nilitoa TV Set ofisini kwangu na kuileta kwenye ukumbi wa mikutano wa klabu, ili kile nnachokiongea kipate legitimacy na sio kuleta porojo za mtaani.

Bahati mbaya sana wale wakosoaji badala ya kujikita na hoja zangu, wakaamua kunishambulia binafsi, na hata walipoamua kujibu hoja waliegemea kishabiki zaidi, huku wakiangalia dhamira za wachezaji bila kuangalia uhalisia wa kisheria na matakwa ya pigo la penati linatolewaje!!

Ndugu zangu mmoja ktk wachambuzi hao alidiriki kusema huko nyuma, pale tuliponyimwa goli liliofungwa na Laudit Mavugo, siku tulipocheza na Stand United, eti mwamuzi alipitiwa, mtu huyo huyo kwenye maonevu dhidi ya hao hao Stand akasema mfanano wa jezi ndio ulisababisha mwamuzi akosee, lakini kwa mechi ya juzi akasema wachezaji hawakuwa na dhamira ya kushika, sijui kwake yy dhamira ina tafsiri gani?unaufata mpira uliojuu unasema dhamira!!

Lau angekuwa mchambuzi mpya ambae kila uchwao yy ni kutuhumu na kuishutumu Simba, ningepata tabu,lakini ni yule yule wa siku zote, na ambae katika kutafuta uungwaji mkono na walio wengi akataka kuhusisha waandishi wote ili kupata moral authoriry na mob support toka kwa wanahabari wengine ambao wengi wao tunafanya kazi nao vzuri sana.

Mchambuzi huyu akaenda mbali zaid kwa kutaka kuonyesha mm Haji sina nnalofanya klabuni zaid ya kelele na nimeshindwa hata kuanzisha jarida la klabu.

Ktk dunia ya kisasa na inayosoma zaid mitandao kuliko print media, idara yangu imejikita kwenye magazine za mtandaoni, nadhani anajua kila mwezi tuna jarida maridhawa liliopo kwenye Simba app na ambalo linasomwa na yoyote aliyejiunga na App yetu iliyo na watumiaji wengi kupita App ya klabu yoyote ktk ukanda huu wa Afrika.

Yy mwenyew bwana mchambuzi anajua kwa nn jarida lake bnafsi la michezo lilikufa kifo cha kawaida, utokaje wake ni kama haupo, anatuchuuza klabu kubwa kama Simba ili iingie mkenge.

Nimjibu Haji ana style yake ya ufanyaji kazi, ana utaratibu wake tofauti na yoyote mwingine, kwangu mm nakubaliana kabisa na ripoti iliyoonyesha Simba ndio ina followers wengi kwenye pages zote za social media nchini kwa vilabu, anzia kwenye App,Fb ,Instagram nk, sasa vp bwana mchambuzi anataka kufananisha tui na nazi?

Mbali ya hayo Simba inaongoza kwa kuingiza mapato mengi ya mlangoni kuliko klabu yoyote nchini ndani ya miaka minne ya nyuma ambayo hatukuchukua ubingwa, nimfahamishe jambo hilo halikuja kama uyoga,

Limetengenezwa na kuandaliwa njia zake makhsuus zilizoifanya tuwe juu.

Nimjuze pia ktk dhamana zangu za kiuongozi nimebuni njia za wanasimba wenyewe kujitolea bonus kwa wachezaji pindi timu ikishinda mchezo wa ligi na kombe la Shirikisho, nadhan bwana mchanbuzi hujui kuwa kuna miloni kumi hutolewa kwa kila mchezo ambao Simba hushinda, wanasimba wanajua dhamira na matendo yangu klabuni.

Sio dhamira yangu kujikweza hapa, lakini baadhi ya watu wanaodhani wanaweza kutumia radio wanazopatia mkate kunituhumu na kutaka nionekane mjinga na niwakalie kimya, hyo kwangu ni big NO.

Na ipo siku tena si nyingi ntawaeleza kwa nn bwana mchambuzi anaichukia sana Simba, ilhali yy anajinasibu ni mfuasi wa klabu hii kubwa kabisa, ukimchokoza kitange, Ngamia hakuachi, na soon atanipata.

Kwa muda mrefu sana kila uchwao ni kuichokonoa Simba, akidhani atapata huruma ya baadhi yao, Simba hatujasahau toka issue ya Singano, hatujasaha hata tuhuma zako kwa kocha Loga na kerry, na kwa kuwa wafuasi wa Simba wana ustaarabu wa kutosha hawaangaiki na ww kama ulivuohangaishwa na wanayanga wakiongozwa na Mzee Akilimali, sentesi hii bwana mchambuzi utakuwa umenielewa sana.

Inafika mahali bwana mchambuzi anazungumzia hata pages zangu binafsi na kusema nataka popularity, ajabu wallah, ktk maongezi na andiko lake amekiri mm ni mtu wa futboll na nimeanza kitambo uchambuzi wa Soka wakati yy bado yupo kitaani, sasa vp nitake umaarufu leo?nna uzoefu mkubwa kabla yake wa kukaa nyuma ya camera, lakini atambue kama popularity ilishatafutwa na wazee wangu waliofanya mambo makubwa kwenye mchezo huu murua zaid duniani.

Sihitaji hilo kwa sasa, nnalopigania ni maslah ya Simba,na nafahamu sina uadui hata chembe na Yanga, nnao utani nao wa kiasili, nnao upinzani wa dak tisini na wa jadi, Yanga na Simba c mahasimu ni wapinzani na watani, hilo ulijue mapema bwana mchambuzi wakati huu ukitafuta kuungwa mkono na wanazi wa Yanga.

Mwisho

Niwaombe wanasimba tusikubali kucheza ngoma inayopigwa na watu wa aina hii ambao kwa kila cha Simba ni kibaya na ambao ana dhamira ya kuichafua taswira ya klabu.

Wahindi wana msemo wao, “Deka jahega”; weka akiba, Ngamia yu macho kuangalia ndege wake, sitahangaika tena na ww, ila tambua twajua mengi.

De la Boss

Thibaut Courtois: Kuishinda Man Utd ni lazima
Essam El Hadary apambanishwa na vijana tuzo ya Afrika 2017