Mkuu wa idara ya habari na mawasilino ya klabu ya Simba Haji Sunday Ramadhan Manara amesema masuala yanayohusu uwekezaji kwenye klabu hiyo yanawahusu Wanachama na Mashabiki wa Simba.

Siku za karibuni baadhi ya vyombo vya habari hasa redio zimekuwa zikiendesha vipindi vya mijadala ambapo moja ya mijadala hiyo ilihoji hatma ya Bilioni 20 ambazo mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ aliahidi kuziweka kwenye akaunti ya mabingwa hao wa nchi baada ya mchakato mzima wa uwekezaji kukamilika.

Manara amesema kimsingi wapenzi, wanachama na mashabiki wa Simba ndio wenye uhalali wa kuhoji masuala yanayoihusu klabu yao na sio kila mtu afanye hivyo kwa utashi wake.

“Wenye uhalali wa kuhoji kuhusu Bilioni 20 za mwekezaji wa Simba ni mashabiki wenyewe ambao walimpa timu, siyo mtu mwingine tu ambaye hana uhalali,” amesema Manara

Mo alishinda zabuni ya uwekezaji kunako klabu ya Simba mwaka 2017 akinunua hisa asilimia 49 kwa kiasi hicho cha fedha.

Tangu wakati huo Mo amekuwa ndiye msimamizi mkuu wa klabu ya Simba akilipa mishahara ya wachezaji pamoja na kununua wachezaji wapya.

Ummy: Viongozi wa dini epukeni misongamano wakati wa Pasaka
Makonda: ''kaka yangu kigwangalla achana na mitandao''