Uongozi wa klabu ya Simba umetoa taarifa za maendeleo ya mshambuliaji kutoka nchini Uganda Emmanuel Anord Okwi, kufuatia majeraha aliyoyapata katika mchezo wa jana wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Okwi alishindwa kuendelea na mchezo huo uliomalizika kwa Simba kupata mabao matatu kwa sifuri, baada ya kupigwa ngumi kwenye koo na mchezaji wa Ruvu Shooting.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na uongozi wa Simba SC kupitia kwa daktari wa kikosi chao, Okwi alishindwa kupumua na kulazimisha Kocha Pierre Lechantre kulazimika kumpumzisha.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema mchezaji huyo anaendelea vizuri ingawa alishindwa kupumua baada ya tukio hilo.

“Alipata maumivu baada ya kupigwa ngumi, unajua ngumi ya kisukusuku kwenye koromeo si jambo dogo.

“Lakini tunashukuru anaendelea vizuri na tunatarajia tutakuwa naye kambini maandalizi dhidi ya Azam,” alisema.

Okwi alitolewa baada ya kupigwa kwa makusudi na beki huyo na Ruvu Shooting walicheza kindava wakionekana walikuwa wamepania kuwaumiza wachezaji wa Simba kama ambavyo walicheza kindava katika mechi dhidi ya Yanga ambayo walilala kwa bao 1-0 lakini mshambuliaji Yohana Nkomola naye alitolewa baada ya kuumizwa na hadi sasa ni majeruhi.

Samaki waliovuliwa kinyemela wapigwa bei
Agrey Moris: Tutaisimamisha Simba SC

Comments

comments