Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba ameuagiza upande wa mashtaka katika kesi ya kutumia lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli, inayomkabili mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee kuhakikisha wanapeleka mashahidi mahakamani ili iweze kumalizika ndani ya mwaka huu.

Ameyasema hayo mara baada ya upande huo kushindwa kupeleka shahidi aliyepangwa kusikilizwa jana, lakini haikuweza kuendelea kutokana na maadhimisho ya siku ya Maulid ambayo kitaifa huwa ni mapumziko.

Kwa mujibu wa taratibu za kimahakama, kesi hiyo ilibidi iendelee siku inayofuata ambayo ni leo, lakini ikashindikana kutokana na shahidi kutofika, ambapo Hakimu Simba amepanga kesi hiyo kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo, Disemba 10 na 11, wakati Mahakama itakaposikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka.

Aidha, Mdee ambaye analiongoza Jimbo la Kawe kwa kipindi cha pili mfululizo, alifikishwa mahakamani Julai 10, 2017 kwa tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi ya Rais na yupo nje kwa dhamana.

Upande wa mashtaka unadai kuwa Julai 3,2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Mdee alitamka kuwa Rais Magufuli “anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afungwe breki”.

Tayari mashahidi watatu wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo wameshatoa ushahidi wao, akiwemo Batseba Kasanga, ambaye ni mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 22, 2018
Andres Iniesta: Dembele ana uwezo mkubwa

Comments

comments