Kesi inayo mkabili Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva pamoja na makamu wake Geofrey Nyange Kaburu,imetajwa tena hii Leo katika Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar esaalaam.

Katika kesi hiyo jopo la mawakili wa upande wa Jamuhuri likiongozwa na Leonard Swai waliomba kusogezwa mbele tarehe ya kusikilizwa kesi hiyo kutokana na upelelezi kutokamilika.

Swai alisema wamepelekan taarifa katika jeshi la polisi kutokana na kesi hiyo kuhusishwa na masuala ya fojari, hivyo wanachokisubiri kwa sasa ni taarifa kutoka katika jeshi hilo.

Hata hivyo kwa upande wa utetezi ukiongozwa na Mutakyamirwa Phelemon pamoja na Evodias Mtawala wameomba kuharakishwa kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Naye Hakimu anayeendesha kesi hiyo Victoria Nongwa, amelitaka jopo la mawakili wa jamuhuri kujitahidi kukamilisha upelelezi juu ya watuhumiwa hao ili kufahamu kama wana makosa ya kujibu mbele ya mahakama hiyo.

Aveva na kaburu walifikishwa mahakamani hapo Julai 3 mwaka huu na kusomewa mashtaka 5 yakiwemo ya kujilipa madeni ya kiasi cha dola za kimarekani 300,000 na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)

Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 30 mwezi huu, na watuhumiwa wamerudishwa tena rumande hadi tarehe ya kutajwa kwa kesi hiyo.

Video: Wanafunzi 106 wavamia sherehe na kujeruhi watu vibaya
Video: Dkt. Mwakyembe awaweka mtegoni BAKITA