Umoja wa Mataifa (UN), umesema una wasiwasi juu ya kukosekana kwa matarajio ya kuanza tena kwa juhudi za mazungumzo ya kidiplomasia yanayohusu kumalizika kwa vita vya Urusi nchini Ukraine.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya siasa kwenye Umoja wa Mataifa, Rosemary Di Carlo, wakati akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama la umoja huo jijini New York nchini Marekani.

Amesema, “Vitisho vya upanuzi wa kijiografia wa mzozo na kunyimwa haki ya utaifa kwa haviendani na ari ya mazungumzo ya Istanbul kuhusu nafaka n a zoezi hili linaonekana halina muafaka kitu kinachoonesha hakuna dalili ya kumalizika kwa vita.”

Katika hotuba yake, Bi. DiCarlo ameielezea hali ya Ukraine kuwa ni ya ugumu kibinadamu na inayozidi kuzorota nchini Ukraine huku vifo vya raia, mamilioni ya wakimbizi, uharibifu mkubwa wa miundombinu ya kibinadamu na miundombinu ya kitamaduni ikizidi kushamiri.

Amesema miji ya Kharkiv, Dnipro, Nikolaev, miji ya Donbass, mji mkuu wa eneo la Kirovogad na makazi mengine yanazidi kushambuliwa, huku baadhi ya miji ya Ukraine ikiwa imeharibiwa kabisa.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, hadi kufikia Julai 27, raia 5,237 waliuawa na 7,035 walijeruhiwa nchini Ukraine, kutokana na takwimu zilizothibitishwa lakini kwa uhalisia namba ni kubwa zaidi.

Ameongeza kuwa, vifo vingi vinasababishwa na matumizi ya silaha za milipuko ya masafa mapana katika maeneo yenye watu wengi, huku mashambulizi kwenye vituo vya afya yakiongeza wasiwasi na kuufanya Umoja wa Mataifa uzidi kutafakari.

Hadi Kufikia Julai 25, kulikuwa na mashambulizi 414 kama hayo, ambayo yalisababisha vifo vya watu 85 na wengine 100 kujeruhiwa huku vitu 168 vya muhimu wa kitamaduni viliharibiwa, zikiwemo taasisi 73 za kidini na makumbusho 13.

Kutokana na mashambulizi hayo, taasisi 2,129 za elimu ziliharibiwa na Di Caro amesema, “Mashambulizi ya kiholela dhidi ya raia na miundombinu ya kiraia ni wazi kuwa ni ukiukaji wa sheria za kibinadamu na sheria za haki za binadamu lakini tunahimiza pande zote za mzozo kuheshimu sheria.”

Mtandao wa Wanawake wavuvi wazinduliwa
Shambulio la bomu uwanjani lauwa 19