Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema licha ya Serikali kupendekeza Bima ya afya kuwa ni lazima, lakini hakuna mwananchi atakayekamatwa au kupigwa faini kwa kutokuwa na hitaji hilo, huku muswada wa sheria ya bima ya afya kwa wote ukitarajia kuanza Julai 2023 baada ya kupitishwa na Bunge.

Ummy, ameyasema hayo hii leo Septemba 27, 2022 jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari na kuongeza kuwa, si lazima Watanzania wote wajiunge na Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF), kutokana na uwepo wa uhuru kwa wananchi kuchagua taasisi waitakayo.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Amesema, “Hakuna Mtanzania atakayefungwa au kukamatwa kwa kutokuwa na bima ya afya, lakini tunawapataje Watanzania ambao hawaumwi kujiunga na bima ya afya, katika hili tumefungamanisha bima ya afya na baadhi ya huduma.”

Aidha, Waziri Ummy, amezitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na leseni ya biashara au leseni ya udereva, na kwamba Serikali inakusudia kuanzisha bima ya afya kwa wote ili kuwapunguzia mzigo wananchi kwenye matibabu na kuzitaja huduma ambazo zitapatikana kwa kila mwananchi kwenye bima ya afya kwa wote kuwa ni CT scan, X Ray na Ultrasound.

Wataka mkataba wa amani, ongezeko la ghasia
Wezi wa Ng'ombe wauwa 11, wamo Polisi wanne