Hit maker wa wimbo unaosumbua spika za mashabiki kutokana na mtindo wake mpya wa uimbaji pamoja na mashairi  ‘Kaa tayari’ Roma Mkatoliki amesema kutokuwa mifumo ya ukaguzi wa nyimbo ndio sababu matatizo ya kufungiwa nyimbo yanakuwa mengi.

Katika mahojiano yake na Bongo5 Roma amesema hakuna kanuni au vyombo vya ukaguzi ambavyo vinachunguza wimbo wa msanii pamoja na mashairi baada ya kutoka studio kabla ya kuufikisha katika chombo cha redio au tv.

”Mfano Msanii anatoka Nachingwea anarekodi studio ya huko hakuna mtu wa kuzipitia lyrics akileta kwenye jamii na watu wakaipokea ndo unaanza kuona vyombo kama Basata,Tcra kumbe vina exist”. Alisema Roma.

Aidha ameongeza kuwa kufungia nyimbo za wasanii pasipo kuwa na sababu za kujitosheleza kuna muumiza msanii huku akiongeza labda nyimbo kufungiwa kwa kosa la maadili ni sawa kwan kuna uwezo wa kuirekebisha lakini siyo kwa kusema wimbo unaleta uchochezi.

”Viva roma viva siwezi kuipafom, nmefungiwa bila kupewa sababu maalumu hata nikiulizwa nakuwa na kigugumizi, mfano tume inaundiwa tume wakati Mwananyamala wanatibu tezi dume mbona tunasikia Wabunge wanaongea au kwasababu wao hawajasemea kwenye mdundo? Alihoji Roma.

Pamoja na hayo ule uvumi wa kuwa Roma alimchana meneja wa diamond ambaye pia anawasimamia wasanii kutoka Tip Top connection kuwa amelitelekeza kundi hilo, amesema lengo lake lilikuwa kukumbusha watu wasisahau wanapotoka.

“Nilichojaribu kumaanisha ni kwamba tusisahau tulikotoka ni kwasababu kuna watu walikuwa wanatutazama, kuna watu walikuwa wanafaidika na kule ambako tumetoka kwahiyo hata baadaye tunakuja kupata mafanikio na kuwekeza nguvu sehemu nyingine, asili kule nyumbani kulikotulea kukatufanya tuwe watu fulani hatupaswi kupasahau,”alisema Roma.

 

 

Kolo Toure: Nitapambana Wakati Wote
FC Barcelona Wakubali Kumsajili Kevin Gameiro