Dhana ya wanawake kupewa kipaumbele kwenye Sheria zinazo angazia maswala ya mahusiano Duniani, kwa kiasi fulani inaaminika ni kama zinatoa nafasi ya ushindi kwa mtoto wakike/Mwanamke endapo litatokea tatizo kati ya Mwanaume na Mwanamke waliokuwa kwenye mahusiano.

Dhana hiyo imemuibua rapa Jack Harlow kutoka nchini Marekani ambaye ameweka wazi hofu yake juu ya majanga ya kushtakiwa yanayowakuta wanaume wengi kuhusu shutuma za unyanyasaji wa kingono na mengine mengi baada ya wapenzi kuachana.

Rapa Jack Harlow ameweka wazi kuwa hivi karibuni ataanza kuwasainisha Wanawake mikataba maalum ya makubaliano kabla ya kuingia kwenye mahusiano na hata wanapoamua kwenda mtoko mahala popote.

Kwa mujibu wa Jarida la GQ ambalo limefanya mahojiano maalum na rapa huyo,  Jack Harlow amesema utamlazimu mwanamke aweke saini ya makubaliano ‘Non-disclosure agreement’ ikiwa kama kiapo cha kutoanika mtandaoni jambo au kitu chochote ambacho kitafanyika baina yao wakiwa kwenye mahusiano au kwenye sehemu yeyote ya starehe.

Vitu vyote vinavyohusisha mawasiliano baina yao ikwa ni pamoja na ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) ambazo watakuwa wakitumiana kupitia simu, zitabaki kuwa siri kati yao, na sio kwa ajili ya kwenda mitandaoni. “mwanamke ambaye hatohitaji kusaini mkataba huo, hata iweje hatopata nafasi ya kuwa na mimi” amesema Jack.

Mapya yaibuka baada ya kifo cha DMX
Ndalichako atoa maagizo Wizarani