Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Bashiru Ally amewaonya wagombea waliopita bila kupigwa kwenye nafasi ya ubunge akiwemo Hamisi Kingwangala na Nape Nnauye kufuata maelekezo ya ratiba ya CCM na kusio kujiamulia.

“Naona Ndg Hamis Kigwangala yupo mitandaoni kujibizana na Mohamed Dewji   mambo ya mipira, tupo kwenye uchaguzi. Nataka nione ana-tweet na wafuasi wake namna Mwenyekiti na Mgombea Urais wetu atakavyoshinda,” amesema.

Bashiru amesema kuwa haingilii maisha binafsi ya mtu ila mgombea yeyote wa CCM anatakiwa kufuata taratibu za chama na si vinginevyo.

“Siingilii maisha binafsi, hakuna maisha binafsi unapokuwa mgombea wa CCM” amesema Bashiru

Aidha amemtaka Nape Nnauye kurudi mkoa Lindi mara moja kumuandalia mkutano raisi mstaafu Jakaya Kikwete ambae anakwenda kunadi sera za chama hicho.

Amesema kuwa “Nimemuona Ndg Nape Nnauye ilemela wakati Ndg Jakaya Kikwete anakwenda Lindi 8/9/2020 kuzindua, anatakiwa awe Lindi kumuandalia Mkutano”

 Bashiru  amesema kuwa viongozi wa chama hicho watakuwa wakali kusimamia nidhamu ya wagombea wa CCM .

Tanzania yapaa kwa ubunifu
Maajabu ya unga wa parachichi