Shirikisho la Soka Barani Ulaya UEFA, limetanganza rasmi wachezaji waliotinga kwenye hatua ya mwisho ya kuwania tuzo ya mchezaji bora barani Ulaya mwaka huu.

Wachezaji waliofanikiwa kuingia kwenye tatu bora ya mwaka huu ni Antoine Griezmann, Gareth Bale na Cristiano Ronaldo.

Orodha ya wachezaji waliofanikiwa kuingia kwenye kumi bora; Luis Suárez (Barcelona), Lionel Messi (Barcelona), Gianluigi Buffon (Juventus),  Pepe (Real Madrid), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Manuel Neuer (Bayern München), Gareth Bale (Real Madrid), Toni Kroos (Real Madrid), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Thomas Müller (Bayern München).

Tuzo hii ambayo itagawiwa kwenye halfa fupi jijini Monaco tarehe 25 Agosti, kwa miaka mitano iliyopita imenyakuliwa na Lionel Messi (2011, 2015), Andrés Iniesta (2012), Franck Ribéry (2013) and Ronaldo (2014).

Everton Kumkosa Muhamed Besic Kwa Miezi Sita
Tamasha La Simba Day Lipo Pale Pale 'Halijapeperushwa'