Mbunge wa Jimbo la Kaliua lililopo mkoani Tabora kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya amesema kuwa hawezi kuhama chama hicho kwasababu yeyote ile kwakuwa hanunuliki na wala hana bei.

Amesema kuwa anafanya kazi kwa misimamo aliyojiwekea na hawezi kutetereka katika nafasi yake, kwani kwa kufanya hivyo atakuwa hawatendei haki wananchi wake waliompigia kura mwaka 2015

Aidha, amesema kuwa anaunga mkono juhudi za Rais Dkt. Magufuli akiwa kwenye chama chake na amefanya hivyo kwenye bajeti za mwaka jana na mwaka huu.

“Mimi nafanya kazi kwa misimamo yangu, penye kukosoa nakosoa penye kusifia nasifia bila woga, hao wanaohama kwa hoja na migogoro ndani ya chama ni waongo kupitiliza hakuna chama chochote kisicho na migogoro lakini ni namna gani ya kukabiliana nao, hata hao CCM wana migogoro kibao lakini wanajua namna ya kuikabili nje wanahisi kuna amani,”amesema Sakaya

Hata hivyo, siku za hivi karibuni,, Magdalena Sakaya alitajwa kwenye orodha ya wabunge watakaohama vyama vyao na kujiunga na CCM, suala ambalo liliibua mijadala kupitia mitandao ya kijamii, ambapo baadhi yao walisema anaweza ondoka pia kutokana na mgogoro wa chama chake cha CUF.

 

Bobi Wine amshukia Kanye West
Rwanda yajipanga kukabiliana na Ebola

Comments

comments