Wanafunzi zaidi ya 20 wanaosoma kidato cha pili hadi cha nne katika shule mbalimbali Mkoani Rukwa, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Nkasi kwa tuhuma za kuwapa ujauzito wanafunzi wa shule za msingi wenye umri mdogo wa kati ya miaka 14 hadi 16.

Hakimu mkazi wa Wilaya ya Nkasi, Ramadhani Rugemalila amesema kuwa wanafunzi waliofikishwa Mahakamani hapo ni 20 na wote wanaumri wa mika 17 wanasoma shule za sekondari.

” Wilaya ya Nkasi changamoto kubwa ya elimu ni suala la mimba za utotoni, wanafunzi wa Sekondari wanawapa mimba wanafunzi wa shule za masingi, katika Mahakama ya Wilaya zipo zaidi ya kesi 20 ambazo watoto wamewapatia watoto wenzao ujauzito” amesema Hakimu Rugemalira.

Amebainisha hayo, alipokuwa akijibu maswali ya wadau wa timu za ulinzi wa watoto kutoka katika kata za Mkumbwa, Mtenga na Nkasi mkoani Rukwa.

Wadau hao wakiwemo madiwani na maofisa elimu kutoka kata hizo tatu, walimu wa shule za msingi na sekondari walitaka kujua sababu ya kutofungwa kwa wahusika wanaowapa mimba wanafunzi hao, licha ya kuwepo mahakamani kesi nyingi za za matukio hayo.

Hakimu huyo alitahadharisha kwamba watuhumiwa hao wana umri chini ya miaka 18 na kwa mujibu wa sheria ya watoto, sheria itawaachia huru na hawatafungwa kwa makosa hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkasi, Missana Kwangura, akizungumza kwenye kikao hicho amesema zaidi ya ya wanafunzi 200 wameacha masomo kwa kipindi cha nusu mwaka huu baada ya kupewa ujauzito.

Naye Ofisa Elimu Kata ya Mkwamba, Andrew Lukuta ameshauri Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi itunge sheria ndogo ili kukomesha mimba za utotoni kwa wasichana wanaosoma.

 

Tahadhari 4 za kujikinga na ugonjwa sugu UTI
Njia zilizotumika zamani kuzuia kushika mimba, kinyesi cha mamba cha tajwa