Kila mwaka ndege aina ya korongo Weupe, Korongo Mayobwe na Mbayuwayu wa Bluu,wanahamia katika hifadhi ya Taifa Kitulo mwezi Novemba na kuondoka Aprili, ambao hutoka katika nchi za Ulaya na Afrika magharibi, lakini kwa mwaka huu mabadiliko ya hali ya hewa yameathiri zoezi hilo.

Hayo yameelezwa na kaimu mhifadhi kuu wa hifadhi ya taifa kitulo, Frank Mapunda alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama cha waandishi wa habari za utalii na uwekezaji Tanzania(TAJAT).

Mpunda amesema mabadiliko ya tabianchi yamesababisha kuchelewesha mvua pamoja na uwepo wa baridi kali katika hifadhi hiyo kupunguza kasi ya ujio wa Ndege wanaohama, kwani hadi sasa ni Ndege wachahe ambao tayari wamewasili mwezi Desemba mwakajana.

Aidha ameongeza kuwa kawaida ya mvua katika hifadhi ya Taifa ya kitulo hunyesha Oktoba lakini hadi kufika Novemba mwaka jana bado ilikuwa ikisuasua.

Ndege hao hukimbia nchi za Ulaya kutokana na baridi kali ambapo huenda kitulo kutokana na haliya hewa kuwanzuri na uwanda mpana unaowawezesha kupata malisho na kuzaliana, kwani hawapendi misitu minene kama ilivyo nchi ya congo hivyo hukimbilia Kitulo kutokana na kuwa na uwanda mweupe usiokuwa na misitu.

Hivi sasa hifadhi hiyo inakuwa kutokana na mikakati inayoendelea kutekelezwa ikiwemo uingizaji wa wanyama na uimarishaji wa miundo mbinu.

 

Wasanii Zanzibar walilia Mradi wa TACIP
Listi ya Mdee viongozi bora CCM 2018

Comments

comments