Spika wa Bunge, Job Ndugai ametangaza kuwa Mbunge aliyekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona mwezi uliopita anaendelea vizuri na anasubiri vipimo vya mwisho ili aruhusiwe.

Katika hatua nyingine, licha ya Chadema kuwataka Wabunge kutohudhuria vikao ili kujikinga na virusi vya corona, Wabunge David Silende (Momba), Joseph Selasini na Peter Lijualikali (Kilombero) wa Chadema wamehudhuria Bungeni leo.

Hii inakuja siku chache tu baada ya mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani, Ester Bulaya kusema hali ya Corona ni mbaya na wabunge wa Chama hicho wamekubaliana kutohudhuria vikao vya Bunge na kujiweka karantini.

Hadi sasa Tanzania ina wagonjwa 480 wa covid – 19, vifo 16 na waliopona 167. kwamujibu wa takwimu zilizotolewa mara ya mwisho Aprili 28, 2020.

Ndege ya vifaa vya covid-19 yaanguka Somalia sita wafariki
Ngoma za Diamond kuanza kupigwa Clouds, Yope remix yafungulia