Serikali ya Ethiopia imetangaza hali ya tahadhari siku moja baada ya waziri mkuu wa nchi hiyo kujiuzulu katika nyadhifa zake zote za chama na serikali.

Katika taarifa iliyotolewa na televisheni ya taifa imesema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kukabiliana na misururu ya maandamano dhidi ya serikali.

Aidha, maelfu ya watu wameuawa na wengine zaidi kujeruhiwa wakati wa maandamano hayo yaliyoitishwa kwa ajili ya kupigania kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa.

Hali hiyo Imejiri siku moja baada ya waziri mkuu, Hailemariam Desalegn kutangaza kuwa anajiuzulu kutokana na mzozo wa kisiasa ambao umeikumba nchi hiyo.

Hata hivyo, Bunge la nchi hiyo linatatarajiwa kuidhinisha kujiuzulu kwa waziri huyo ambako tayari kumeungwa mkono na chama tawala.

Salum Mwalimu: Niko tayari kupoteza maisha kuliko kuibiwa kura
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 17, 2018