Jeshi la Polisi Wilayani Bukoba Mkoani Kagera limemuachia kwa dhamana mwenyekiti wa baraza la wanawake CHADEMA Taifa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe Jijini Dar es salaam, Halima Mdee aliyekuwa ameshikiliwa alipokuwa akifanya kikao chake cha ndani na wanachama wenzake.

Akizungumza na waandishi baada ya kuachiwa huru kwa mbunge huyo, katibu mkuu wa baraza hilo, Grace Tendega amesema kuwa walienda wilayani Bukoba kufanya kikao chao cha ndani kwaajili ya kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni ndipo walipokamatwa na polisi na kuwaambia wanawahitaji viongozi hao.

Aidha, Tendega ameongeza kuwa walipofika polisi walionyeshwa baadhi ya meseji ambazo zilidaiwa kuwa, Mdee alitoa maneno ya kashifa kwa serikali katika kikao hicho na kusema kuwa wao vitu hivyo havikutamkwa wala havikuzungumzwa.

Pia, ameongeza kuwa kuwa baada ya kuandika maelezo wabunge watatu waliachiwa kwa dhamana ambapo Mdee hakuachiwa na kulala kituo cha polisi Bukoba hadi hapo jana alipoachiwa baada ya kudhaminiwa na Meya wa Manispaa ya Bukoba pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bukoba, Wilfredy Lwakatale na kupewa mwezi mmoja pale watakapo muhitaji watamuomba arudi Bukoba.

Hata hivyo, Tendega amesema kuwa walifanya mkutano wao kwa amani bila vurugu wala kusumbuliwa licha ya mbunge Mdee kusumbuliwa na maradhi baada ya kufanyiwa upasuaji hivi karibuni.

LIVE MWANZA: Rais Magufuli akifanya ziara ya Ukaguzi katika Bandari jijini Mwanza
Zuma alia na hujuma, 'Wanampango wa kunipoteza kisiasa'